01
Utangulizi
Nuru ni lugha ya kiprogramu inayotumia maneno ya Kiswahili. Kamusi hii inaeleza kila sehemu ya lugha kwa mifano mifupi. Bonyeza Jaribu kwenye mfano wowote ili uufungue Uwanjani, uubadilishe na uuendeshe.
andika("Habari, Dunia!")Matokeo
Habari, Dunia!
andika() huchapisha thamani moja au zaidi. Ukiweka thamani kadhaa, Nuru huziweka nafasi katikati.
andika("Nina miaka", 12)
andika(3 + 4)Matokeo
Nina miaka 127
Maoni
Maoni ni maelezo kwa ajili ya binadamu, na Nuru huyaruka. Tumia // kwa mstari mmoja na /* ... */ kwa mistari mingi.
// Huu ni mstari wa maoni
andika("Maoni hayachapishwi")
/*
Maoni ya mistari
mingi
*/Matokeo
Maoni hayachapishwi
02
Vibadilika
Kibadilika ni jina linalohifadhi thamani. Kiunde kwa fanya. Baadaye unaweza kukipa thamani mpya bila fanya.
fanya jina = "Amani"
fanya umri = 12
andika(jina, "ana miaka", umri)
umri = 13
andika(jina, "sasa ana miaka", umri)Matokeo
Amani ana miaka 12Amani sasa ana miaka 13
Jina la kibadilika huanza na herufi au _, na linaweza kuwa na namba: alama1, jina_kamili. Herufi kubwa na ndogo ni tofauti, kwa hiyo Jina si sawa na jina. Usitumie maneno ya Nuru kama kama au kwa kuwa majina.
Njia fupi
Kubadilisha thamani ya kibadilika kwa kutumia thamani yake ya zamani ni jambo la kawaida, kwa hiyo Nuru ina njia fupi: +=, -=, *=, ++ na --.
fanya alama = 10
alama += 5 // 15
alama++ // 16
alama -= 2 // 14
alama *= 2 // 28
andika(alama)Matokeo
28
03
Aina za data
Kila thamani ina aina. Ukitaka kujua aina ya thamani, iulize Nuru kwa aina().
| Aina | Mfano | Maana |
|---|---|---|
NAMBA | 42, -7 | namba kamili |
DESIMALI | 3.14, 0.5 | namba yenye nukta |
NENO | "Habari" | maandishi ndani ya alama za nukuu |
BOOLEAN | kweli, sikweli | ndiyo au hapana |
TUPU | tupu | hakuna thamani |
ORODHA | [1, 2, 3] | vitu vilivyopangwa kwa mfuatano |
KAMUSI | {"jina": "Amani"} | funguo na thamani zake |
andika(aina(42))
andika(aina(3.14))
andika(aina("Habari"))
andika(aina(kweli))
andika(aina(tupu))
andika(aina([1, 2, 3]))
andika(aina({"jina": "Amani"}))Matokeo
NAMBADESIMALINENOBOOLEANTUPUORODHAKAMUSI
Kubadilisha aina
namba() hugeuza thamani kuwa NAMBA, tungo() huigeuza kuwa NENO, na badilisha(thamani, "AINA") huigeuza kuwa NAMBA, DESIMALI, NENO au BOOLEAN.
andika(namba("42") + 1)
andika(tungo(42) + "!")
andika(badilisha("3.5", "DESIMALI"))
andika(namba(3.9)) // sehemu ya desimali inaondolewaMatokeo
4342!3.53
Dokezo: Ukichapisha tupu, Nuru huonyesha null.
04
Waendeshaji
Waendeshaji hufanya hesabu, hulinganisha thamani na huunganisha masharti.
Hesabu
| Mwendeshaji | Kazi | Mfano |
|---|---|---|
+ | jumlisha | 2 + 3 → 5 |
- | toa | 9 - 4 → 5 |
* | zidisha | 3 * 4 → 12 |
/ | gawanya | 7 / 2 → 3.5 |
% | baki ya kugawanya | 7 % 2 → 1 |
** | kipeo | 2 ** 3 → 8 |
andika(7 / 2)
andika(8 / 2)
andika(7 % 2)
andika(2 ** 3)
andika(2 + 3 * 4)
andika((2 + 3) * 4)Matokeo
3.54181420
Kuzidisha na kugawanya hufanyika kabla ya kujumlisha na kutoa. Tumia mabano ( ) ukitaka mpangilio mwingine.
Kulinganisha
| Mwendeshaji | Maana | Mfano |
|---|---|---|
== | ni sawa na | 5 == 5 → kweli |
!= | si sawa na | 5 != 3 → kweli |
< > | ndogo kuliko, kubwa kuliko | 3 < 5 → kweli |
<= >= | ndogo au sawa, kubwa au sawa | 5 >= 6 → sikweli |
Mantiki
| Mwendeshaji | Maana | Mfano |
|---|---|---|
&& | na: zote mbili ni kweli | kweli && sikweli → sikweli |
|| | au: moja wapo ni kweli | kweli || sikweli → kweli |
! | si: hugeuza jibu | !kweli → sikweli |
fanya umri = 14
andika(umri >= 13 && umri <= 19)
andika(umri < 5 || umri > 60)
andika(!(umri == 14))Matokeo
kwelisikwelisikweli
Maneno na ktk
+ huunganisha maneno mawili, na * hurudia neno. ktk (yaani "katika") huuliza kama kitu kipo ndani ya orodha, neno au kamusi.
andika("Nuru" + " " + "Programu")
andika("ha" * 3)
andika(2 ktk [1, 2, 3])
andika("jina" ktk {"jina": "Amani"})Matokeo
Nuru Programuhahahakwelikweli
Dokezo: Huwezi kujumlisha NENO na NAMBA moja kwa moja. Geuza namba kuwa neno kwanza: "Umri: " + tungo(12).
05
Maamuzi
Programu hufanya maamuzi kwa kama. Ongeza au kama kwa hali nyingine, na sivyo kwa kila kitu kilichobaki.
fanya alama = 72
kama (alama >= 80) {
andika("Daraja A")
} au kama (alama >= 60) {
andika("Daraja B")
} sivyo {
andika("Jaribu tena")
}Matokeo
Daraja B
Hali huandikwa ndani ya mabano ( ), na kila tawi ndani ya { }. Nuru hukagua hali moja baada ya nyingine na huendesha tawi la kwanza lililo kweli tu.
badili, ikiwa, kawaida
Ukilinganisha thamani moja na chaguo nyingi, badili husomeka vizuri kuliko kama nyingi. Kila ikiwa inaweza kuwa na thamani kadhaa zilizotenganishwa kwa koma, na kawaida hushika kila kitu kingine.
fanya siku = "Jumamosi"
badili (siku) {
ikiwa "Jumamosi", "Jumapili" {
andika("Ni wikendi!")
}
ikiwa "Ijumaa" {
andika("Wikendi inakaribia")
}
kawaida {
andika("Siku ya shule")
}
}Matokeo
Ni wikendi!
06
Vitanzi
Vitanzi hurudia kazi. wakati hurudia maadamu hali ni kweli. kwa ... ktk hupitia kila kitu ndani ya orodha, neno au kamusi.
wakati
fanya i = 0
wakati (i < 5) {
i++
andika(i)
}Matokeo
12345
Dokezo: Hakikisha hali itakuwa sikweli siku moja, la sivyo kitanzi hakitaisha. Uwanjani, bonyeza Simamisha kusimamisha programu iliyokwama.
kwa ... ktk
fanya matunda = ["embe", "papai", "nanasi"]
kwa tunda ktk matunda {
andika("Napenda", tunda)
}Matokeo
Napenda embeNapenda papaiNapenda nanasi
Ukiweka majina mawili, la kwanza hupata nafasi (kuanzia 0) na la pili hupata kitu chenyewe.
fanya matunda = ["embe", "papai", "nanasi"]
kwa i, tunda ktk matunda {
andika(i, tunda)
}Matokeo
0 embe1 papai2 nanasi
kwa herufi ktk "Nuru" {
andika(herufi)
}Matokeo
Nuru
mfululizo
mfululizo() hutengeneza orodha ya namba, na ni rafiki mkubwa wa kwa. Namba ya mwisho haihusishwi.
| Mwito | Matokeo |
|---|---|
mfululizo(5) | [0, 1, 2, 3, 4] |
mfululizo(1, 6) | [1, 2, 3, 4, 5] |
mfululizo(0, 10, 3) | [0, 3, 6, 9] |
mfululizo(5, 0, -1) | [5, 4, 3, 2, 1] |
kwa i ktk mfululizo(1, 6) {
andika(i, "x", i, "=", i * i)
}Matokeo
1 x 1 = 12 x 2 = 43 x 3 = 94 x 4 = 165 x 5 = 25
vunja na endelea
vunja hutoka nje ya kitanzi mara moja. endelea huruka sehemu iliyobaki ya mzunguko huu na kwenda mzunguko unaofuata.
kwa n ktk mfululizo(1, 11) {
kama (n % 2 == 0) { endelea } // ruka namba shufwa
kama (n > 7) { vunja } // simama baada ya 7
andika(n)
}Matokeo
1357
07
Vitendakazi
Kitendakazi ni kipande cha kodi chenye jina, unachoweza kukiita tena na tena. Kiunde kwa unda, na tumia rudisha kurudisha jibu.
fanya jumlisha = unda(a, b) {
rudisha a + b
}
andika(jumlisha(2, 3))
andika(jumlisha(10, 32))Matokeo
542
Hoja zenye thamani ya kawaida
Hoja inaweza kuwa na thamani ya kawaida. Ikiachwa wakati wa kuita, thamani hiyo hutumika.
fanya salimu = unda(jina, salamu = "Habari") {
andika(salamu + ", " + jina + "!")
}
salimu("Amani")
salimu("Neema", "Mambo")Matokeo
Habari, Amani!Mambo, Neema!
Vitendakazi ndani ya vitendakazi
Kitendakazi ni thamani kama nyingine: unaweza kukihifadhi kwenye kibadilika au kukirudisha. Kitendakazi cha ndani hukumbuka vibadilika vya mahali kilipoundwa (closure).
fanya zidishaKwa = unda(n) {
rudisha unda(x) {
rudisha x * n
}
}
fanya mara2 = zidishaKwa(2)
fanya mara10 = zidishaKwa(10)
andika(mara2(7), mara10(7))Matokeo
14 70
Dokezo: Kitendakazi cha ndani kinaweza kusoma vibadilika vya nje, lakini kukipa kibadilika cha nje thamani mpya hakubadilishi kile cha nje.
Kujirudia
Kitendakazi kinaweza kujiita chenyewe. Kila mara kinatatua tatizo dogo zaidi hadi kifike kwenye hali ya msingi.
fanya kipeo = unda(n) {
kama (n <= 1) { rudisha 1 }
fanya kabla = kipeo(n - 1)
rudisha n * kabla
}
andika(kipeo(5))Matokeo
120
Dokezo: Hifadhi jibu la mwito wa kujirudia kwenye kibadilika kwanza, kama kabla hapo juu. Toleo la kivinjari bado lina hitilafu inayosimamisha programu ukiandika rudisha n * kipeo(n - 1) moja kwa moja.
08
Orodha
Orodha huhifadhi vitu vingi kwa mpangilio. Kitu cha kwanza kiko nafasi 0.
fanya rangi = ["nyekundu", "kijani", "bluu"]
andika(rangi[0])
rangi[1] = "njano"
andika(rangi)
andika(rangi[10]) // nafasi isiyokuwepoMatokeo
nyekundu[nyekundu, njano, bluu]null
Vitendakazi vya orodha
| Kitendakazi | Kazi | Mfano |
|---|---|---|
idadi() | idadi ya vitu | [4, 5, 6].idadi() → 3 |
sukuma(x, ...) | ongeza kitu kimoja au zaidi mwishoni | o.sukuma(7) |
yamwisho() | kitu cha mwisho | [4, 5, 6].yamwisho() → 6 |
unga(kitenganishi) | unganisha vitu kuwa NENO moja | [1, 2].unga("-") → 1-2 |
tafuta(x) | rudisha x kama kipo, sivyo tupu | [4, 5].tafuta(5) → 5 |
chuja(unda(x) {...}) | baki na vitu ambavyo kitendakazi kinarudisha kweli | o.chuja(unda(x) { rudisha x > 2 }) |
map(unda(x) {...}) | orodha mpya yenye jibu la kitendakazi kwa kila kitu | o.map(unda(x) { rudisha x * 2 }) |
fanya alama = [70, 85, 40, 92]
andika(alama.idadi())
alama.sukuma(66)
andika(alama)
andika(alama.yamwisho())
andika(alama.unga(" | "))
andika(alama.tafuta(85))
andika(alama.tafuta(100))Matokeo
4[70, 85, 40, 92, 66]6670 | 85 | 40 | 92 | 6685null
fanya alama = [70, 85, 40, 92]
fanya waliofaulu = alama.chuja(unda(a) { rudisha a >= 50 })
fanya zaidi = alama.map(unda(a) { rudisha a + 5 })
andika(waliofaulu)
andika(zaidi)Matokeo
[70, 85, 92][75, 90, 45, 97]
Dokezo: Kitendakazi unachokipa chuja au map kinaona hoja yake tu, si vibadilika vya nje. Andika namba unazohitaji ndani yake moja kwa moja.
Kujumlisha orodha
fanya a = [1, 2]
fanya b = [3, 4]
andika(a + b)
fanya jumla = 0
kwa x ktk a + b {
jumla += x
}
andika("Jumla:", jumla)Matokeo
[1, 2, 3, 4]Jumla: 10
09
Neno
NENO ni maandishi ndani ya alama za nukuu, "hivi" au 'hivi'. Neno lina vitendakazi vyake.
| Kitendakazi | Kazi | Mfano |
|---|---|---|
idadi() | idadi ya herufi | "Nuru".idadi() → 4 |
herufikubwa() | HERUFI KUBWA | "nuru".herufikubwa() → NURU |
herufindogo() | herufi ndogo | "NURU".herufindogo() → nuru |
gawa(kitenganishi) | gawa neno kuwa orodha (kwa kawaida kwenye nafasi) | "a,b".gawa(",") → [a, b] |
panga(...) | jaza nafasi {0}, {1} ... kwa hoja | "Habari {0}".panga("Amani") |
fanya jina = "Nuru Programu"
andika(jina.idadi())
andika(jina.herufikubwa())
andika(jina.herufindogo())
andika(jina.gawa())
andika("embe,papai,nanasi".gawa(","))Matokeo
13NURU PROGRAMUnuru programu[Nuru, Programu][embe, papai, nanasi]
fanya ujumbe = "Habari {0}, una miaka {1}.".panga("Amani", 12)
andika(ujumbe)Matokeo
Habari Amani, una miaka 12.
Dokezo: {0} ni hoja ya kwanza na {1} ni ya pili. Kila hoja unayoipa panga lazima itumike.
Herufi maalum
Ndani ya neno, \n huanzisha mstari mpya na \t huweka nafasi ya tab.
andika("Mstari wa kwanza\nMstari wa pili")Matokeo
Mstari wa kwanzaMstari wa pili
Dokezo: Huwezi kuchukua herufi moja kwa neno[0]. Pitia herufi kwa kwa herufi ktk neno.
10
Kamusi
KAMUSI huhifadhi jozi za ufunguo na thamani. Ufunguo unaweza kuwa NENO, NAMBA, DESIMALI au BOOLEAN.
fanya mwanafunzi = {"jina": "Amani", "darasa": 5}
andika(mwanafunzi["jina"])
mwanafunzi["shule"] = "Uhuru"
mwanafunzi["darasa"] += 1
andika(mwanafunzi["shule"], mwanafunzi["darasa"])
andika(mwanafunzi["simu"]) // ufunguo usiokuwepo
andika("jina" ktk mwanafunzi)Matokeo
AmaniUhuru 6nullkweli
Kupitia kamusi
fanya bei = {"embe": 500, "papai": 1500, "nanasi": 2000}
kwa tunda, shilingi ktk bei {
andika(tunda, "ni shilingi", shilingi)
}Matokeo
embe ni shilingi 500nanasi ni shilingi 2000papai ni shilingi 1500
Dokezo: Usitegemee mpangilio wa funguo. Ukichapisha kamusi nzima au kuipitia, funguo zinaweza kutoka kwa mpangilio tofauti na ulivyoziandika.
Kamusi mbili huunganishwa kwa +: a + b hutoa kamusi mpya yenye funguo za zote mbili.
11
Ingizo: jaza
jaza() huuliza swali na kusubiri mtumiaji aandike jibu. Uwanjani, jibu huandikwa kwenye terminali chini ya programu.
fanya jina = jaza("Jina lako ni nani? ")
andika("Karibu, " + jina + "!")Matokeo· Ukiandika: Amani
Karibu, Amani!
jaza() hurudisha NENO kila mara, hata ukiandika namba. Tumia namba() kabla ya kufanya hesabu.
fanya umri = namba(jaza("Una miaka mingapi? "))
andika("Mwakani utakuwa na miaka", umri + 1)Matokeo· Ukiandika: 12
Mwakani utakuwa na miaka 13
12
Moduli
Moduli ni maktaba ya vitendakazi vya ziada. Ileta kwa tumia, kisha iite kwa nukta: hisabati.sqrt(16).
hisabati
Hesabu za kina: vipeuo, pembe, logi na namba za nasibu.
| Kitendakazi | Kazi | Mfano |
|---|---|---|
PI(), e(), phi() | namba maalum | hisabati.PI() → 3.141592653589793 |
sqrt(x), cbrt(x) | kipeuo cha pili, cha tatu | hisabati.sqrt(16) → 4 |
root(x, n) | kipeuo cha n | hisabati.root(27, 3) → 3 |
abs(x) | thamani bila alama ya hasi | hisabati.abs(-5) → 5 |
sign(x) | -1, 0 au 1 | hisabati.sign(-3) → -1 |
round(x) | kadiria DESIMALI hadi namba kamili | hisabati.round(2.6) → 3 |
floor(x), ceil(x) | shusha, pandisha hadi namba kamili | hisabati.floor(2.9) → 2 |
max(orodha), min(orodha) | kubwa zaidi, ndogo zaidi | hisabati.max([3, 9, 2]) → 9 |
factorial(n) | n! (n × ... × 1) | hisabati.factorial(5) → 120 |
hypot(a, b) | upande mrefu wa pembetatu | hisabati.hypot(3, 4) → 5 |
random() | namba ya nasibu kati ya 0 na 1 | hisabati.random() |
sin, cos, tan, asin, acos, atan | pembe (kwa radiani, DESIMALI) | hisabati.cos(0.0) → 1 |
exp, log, log10, log2 | vipeo na logi (DESIMALI) | hisabati.log2(8) → 3 |
tumia hisabati
andika(hisabati.sqrt(16))
andika(hisabati.PI())
andika(hisabati.max([3, 9, 2]))
andika(hisabati.round(2.6))
andika(hisabati.factorial(5))
andika(hisabati.cos(0.0))Matokeo
43.141592653589793931201
tumia hisabati
fanya kete = hisabati.floor(hisabati.random() * 6) + 1
andika("Kete imeonyesha", kete)Matokeo (mfano)
Kete imeonyesha 4
Dokezo: PI() na e() ni vitendakazi, kwa hiyo weka mabano. Vitendakazi vya pembe, round, exp na log vinapokea DESIMALI tu: andika hisabati.cos(0.0), si hisabati.cos(0).
muda
Saa, tarehe na kusubiri. Muda huandikwa kama saa:dakika:sekunde siku-mwezi-mwaka.
| Kitendakazi | Kazi | Mfano |
|---|---|---|
hasahivi() | muda wa sasa | muda.hasahivi() |
leo() | tarehe ya leo | muda.leo() → 12-10-2026 |
lala(sekunde) | subiri kwa sekunde kadhaa | muda.lala(1) |
tangu(m) | sekunde zilizopita tangu muda m | muda.tangu(mwanzo) |
baada_ya(sekunde) | muda baada ya sekunde kadhaa kuanzia sasa | muda.baada_ya(60) |
tofauti(a, b) | sekunde kati ya nyakati mbili | muda.tofauti(b, a) |
ongeza(m, dakika=5) | ongeza sekunde, dakika, masaa, siku, wiki, miezi au miaka | muda.ongeza(m, siku=1) |
tumia muda
fanya mwanzo = muda.hasahivi()
andika("Leo ni", muda.leo())
muda.lala(1)
andika("Sekunde zilizopita:", muda.tangu(mwanzo))Matokeo (mfano)
Leo ni 12-10-2026Sekunde zilizopita: 1
jsoni
Soma na uandike data ya JSON, muundo unaotumiwa na tovuti nyingi.
| Kitendakazi | Kazi |
|---|---|
dikodi(neno) | geuza JSON kuwa kamusi au orodha |
enkodi(thamani) | geuza kamusi au orodha kuwa JSON |
tumia jsoni
fanya data = jsoni.dikodi("{\"jina\": \"Amani\", \"alama\": [90, 85]}")
andika(data["jina"])
andika(data["alama"])
andika(jsoni.enkodi({"somo": "Nuru"}))Matokeo
Amani[90, 85]{"somo":"Nuru"}
kobe
Kobe ni kasa mdogo anayechora kwenye turubai ya 600 × 600. Anaanzia katikati (0, 0) akielekea mashariki (kulia). y huongezeka kwenda juu. Programu yenye tumia kobe hufunguka Uwanjani pamoja na turubai.
| Kitendakazi | Kazi |
|---|---|
mbele(n), nyuma(n) | sogea mbele au nyuma hatua n |
kulia(digrii), kushoto(digrii) | geuka kulia au kushoto |
elekea(digrii) | elekea upande fulani: 0 mashariki, 90 kaskazini |
nenda(x, y) | nenda moja kwa moja hadi (x, y) |
nyumbani() | rudi katikati ukielekea mashariki |
kalamu_juu(), kalamu_chini() | inua kalamu (sogea bila kuchora), ishushe |
rangi(r) | rangi ya kalamu |
rangi_ya_ndani(r) | rangi ya kujaza maumbo |
anza_kujaza(), maliza_kujaza() | anza umbo, kisha lipake rangi ya ndani |
unene(n) | unene wa mstari |
duara(r) | chora duara lenye nusukipenyo r kuzunguka kobe |
nukta(ukubwa) | weka nukta |
maandishi(neno, ukubwa) | andika maneno kwenye turubai |
mandhari(r) | rangi ya turubai |
kasi(n) | kasi ya kuchora: 0 papo hapo hadi 10 |
futa() | safisha turubai |
ficha(), onyesha() | ficha au onyesha kobe |
mahali() | rudisha [x, y] |
mwelekeo() | rudisha mwelekeo kwa digrii |
Rangi: nyeusi, nyeupe, nyekundu, kijani, bluu, samawati, njano, machungwa, zambarau, waridi, kahawia, kijivu, dhahabu, fedha, au msimbo kama "#ff8800".
tumia kobe
kobe.rangi("bluu")
kobe.unene(4)
kwa i ktk mfululizo(4) {
kobe.mbele(150)
kobe.kulia(90)
}
andika(kobe.mahali())Matokeo
[0, 0]
Angalia turubai ya kobe.
tumia kobe
kobe.rangi("nyekundu")
kobe.rangi_ya_ndani("njano")
kobe.nenda(-100, 30)
kobe.anza_kujaza()
kwa i ktk mfululizo(5) {
kobe.mbele(200)
kobe.kulia(144)
}
kobe.maliza_kujaza()Matokeo
Hakuna maandishi. Angalia turubai ya kobe.
tumia kobe
fanya rangi = ["nyekundu", "machungwa", "njano", "kijani", "bluu", "zambarau"]
kobe.kalamu_juu()
kwa i, r ktk rangi {
kobe.nyumbani()
kobe.elekea(i * 60)
kobe.mbele(120)
kobe.rangi(r)
kobe.nukta(50)
}
kobe.nyumbani()
kobe.rangi("nyeusi")
kobe.maandishi("Nuru", 28)Matokeo
Hakuna maandishi. Angalia turubai ya kobe.
ubao
Ubao ni bodi ya elektroniki ya kuigiza: taa 8 (namba 1 hadi 8), kengele na skrini ndogo ya mistari 2 yenye herufi 16 kila mstari. Ni hatua ya kwanza kabla ya kushika vifaa halisi.
| Kitendakazi | Kazi |
|---|---|
washa(n), zima(n) | washa au zima taa namba n |
geuza(n) | badilisha hali ya taa |
washa_zote(), zima_zote() | washa au zima taa zote |
imewaka(n) | rudisha kweli kama taa imewaka |
rangi(n, r) | rangi ya taa n |
kengele(hz, ms) | piga kengele: sauti kwa Hz, muda kwa milisekunde |
skrini(neno) | andika kwenye skrini ndogo |
subiri(ms) | subiri milisekunde kadhaa |
tumia ubao
ubao.skrini("Taa zinawaka")
kwa i ktk mfululizo(1, 9) {
ubao.washa(i)
ubao.subiri(150)
}
ubao.kengele(880, 300)
ubao.zima_zote()Matokeo
Hakuna maandishi. Angalia ubao.
tumia ubao
ubao.rangi(1, "nyekundu")
ubao.rangi(2, "njano")
ubao.rangi(3, "kijani")
kwa taa ktk [1, 2, 3] {
ubao.washa(taa)
ubao.subiri(700)
ubao.zima(taa)
}
andika(ubao.imewaka(3))Matokeo
sikweli
Angalia ubao.
13
Makosa ya kawaida
Nuru hueleza makosa kwa Kiswahili na hutaja mstari ulipotokea. Haya ndiyo utakayoyaona mara nyingi.
| Ujumbe | Maana yake | Rekebisha |
|---|---|---|
Neno Halifahamiki: x | umetumia jina ambalo halijaundwa | liunde kwa fanya kwanza, au angalia tahajia |
Aina Hazilingani: NENO + NAMBA | umechanganya aina mbili zisizoendana | geuza kwa tungo() au namba() |
Operesheni Haieleweki: NENO < NENO | mwendeshaji huu haufanyi kazi na aina hii | tumia mwendeshaji mwingine |
Tulitegemea kupata ), badala yake tumepata MWISHO | mabano hayajafungwa; MWISHO ni mwisho wa kodi | |
Hukufunga Mabano '}' | { haina } yake | ongeza } |
Tulitegemea kupata (, badala yake tumepata KITAMBULISHI | kama au wakati bila mabano ( ) | andika kama (x > 3) { ... } |
Hiki sio kiendesha: NAMBA | umeita kitu ambacho si kitendakazi | |
Tumekosa Hoja | kitendakazi kimeitwa na hoja chache kuliko inavyohitaji | |
Samahani, kiendesha hiki hakitumiki na tungo (Neno) | kitendakazi hicho hakipo kwa orodha au neno hili | angalia majedwali ya Orodha na Neno |
Haiwezi kubadilisha 'abc' kuwa NAMBA | namba() imepewa maandishi yasiyo namba | |
Moduli sayari haipo | hakuna moduli yenye jina hilo | angalia sehemu ya Moduli |
Hoja lazima iwe desimali | kitendakazi cha hisabati kinahitaji DESIMALI | andika 0.0 badala ya 0 |
Maneno machache yanajirudia kwenye ujumbe: Mstari ni namba ya mstari, Hoja ni thamani unayokipa kitendakazi, KITAMBULISHI ni jina, na HARAMU ni herufi ambayo Nuru haiijui.
fanya jina = "Amani"
andika(Jina)Matokeo
Kosa: Mstari 2: Neno Halifahamiki: Jina
fanya umri = 12
andika("Umri: " + umri)Matokeo
Kosa: Mstari 2: Aina Hazilingani: NENO + NAMBA
fanya x = 5
kama x > 3 {
andika("kubwa")
}Matokeo
Kuna makosa yafuatayo:Mstari 2: Tulitegemea kupata (, badala yake tumepata KITAMBULISHIMstari 3: Tulitegemea kupata :, badala yake tumepata }Mstari 4: Tumeshindwa kuparse }
Dokezo: Kosa moja la sintaksia linaweza kuleta jumbe kadhaa. Rekebisha ujumbe wa kwanza, kisha endesha tena.